Jenga
mti wa familia
Una hamu kuhusu nasaba yako? Anza mara moja utafutaji wako wa nasaba BURE katika mti wa familia wa jamii ya ulimwenguni kote. Unganika sasa—Yawezekana tayari tuna maelezo kuhusu familia yako.

Jinsi unavyofanya kazi
Hatua ya 1:
Ingia na ongeza kile unachojua.
Kijenzi cha mti kitakuongoza. Utaanza kwa kuongeza wazazi wako na mababu zako. Usijali—taarifa zote za watu walio hai zinawekwa faragha.
Hatua ya 2:
Tutatafuta kwa ajili ya miunganiko ya familia yako.
Unapoongeza taarifa, mfumo utaanza kutafuta wanafamilia yako kutoka kwenye mti wa jamii na kutoka kwenye kumbukumbu za kihistoria, kama vyeti vya kuzaliwa na vifo.
Hatua ya 3:
Tazama mti wa familia yako ukikua!
Mti wa jumuiya wa familia utahamasisha ugunduzi wakati unapoongeza matawi kwenye mti wako. Mti wako unapokua, utajifunza zaidi kuhusu familia yako na kuhisi muunganiko wa karibu na waliopita.
Anzisha Mti Wako
Kwa nini utumie Mti Shirikishi wa FamilySearch?
Tumia nguvu ya ulimwenguni kote, ukoo uliopatikana na kundi kubwa ili kugundua hadithi ya familia yako.
Mti wa Familia Mkubwa Zaidi Ulimwenguni wa Mtandaoni
Wale wanaoanza Mti wa Familia kwenye FamilySearch sio tu kwamba wanaiweka pamoja hadithi ya familia yao—wanachangia kutengeneza mti wa familia ya binadamu ulimwenguni kote uliyounganika.
Imeshirikiwa na Inafikiwa Kiurahisi
Mti uliotolewa wa FamilySearch una wasifu mmoja wa umma kwa ajili ya mtu binafsi aliyefariki, ukitengeneza mahali pamoja kwa ajili ya taarifa zote zilizotolewa badala ya kusambazwa kote katika miti mingi. Hii pia huongeza faragha.
Jenga Mti Wako kwa Urahisi
Mara tu unapoongeza jamaa aliyefariki kwenye mti, FamilySearch itajaribu kukuunganisha kwenye habari yoyote iliyonayo toka data yake kuhusu mtu huyo. Kama inapata uoanisho, FamilySearch inaweza kujaza habari yenyewe, na kukuokolea muda sana!
Shirikiana na Wengine
Mti wa Familia wa FamilySearch unawawezesha wazao wote kushiriki taarifa ambazo wengine yawezakuwa hawazifahamu na unatoa vyanzo ili kuthibitisha usahihi wa taarifa. Matokeo ya jumla ya mti shirikishi yanaweza kuwa kamili na sahihi zaidi kuliko miti binafsi.
Unganika na Wanafamilia Wengine
Kufanya kazi kwa pamoja kwenye mti wa ulimwenguni kote pia kunawasaidia wazao kuungana mmoja na mwingine. Unaweza kumpata jamaa yako aliyetembelea makaburi sawa na hayo, aliyeuliza maswali sawa na hayo—na hata aliyejifunza kupenda au aliyevutiwa na—mababu hao hao.
Ijaribu sasa.
Anza na kile unachokijua. Tutakusaidia kujaza nafasi wazi.
Mti wa familia ni nini?
Ufafanuzi:
Mti wa familia ni wasilisho la picha ya familia pana, yenye kujikita kwenye majina, tarehe, mahali na mahusiano. Huonyesha jinsi watu binafsi wanavyounganika kupitia vizazi tofauti.
Soma ZaidiMaswali ya mara kwa mara
Mti wa Familia wa FamilySearch
Unatumika bila malipo na ni rahisi kuanza. Ugunduzi unakusubiria.
