Ordinances Ready:
Pokea Majina ya kupeleka Hekaluni
Wakusanye mababu zako kwa Kristo kupitia maagano matakatifu ya hekaluni.

Ordinances Ready ni nini?
Ordinances Ready inahakikisha una jina la kupeleka hekaluni—kila wakati. Kwa kubofya mara kadhaa tu, inatafuta mti wako wa familia na vyanzo vingine na mara moja hukupa majina ili uweze kufokasi kwenye kile kilicho cha muhimu zaidi: kusogea karibu na Mwokozi kupitia huduma za hekaluni.
Ninatumiaje Ordinances Ready?
Chagua mwanamume au mwanamke.
Chagua ibada unayotaka kufanya.
Chapisha kadi nyumbani au hekaluni.
Pokea majina yaliyo tayari kwa ajili ya hekalu sasa.
Ni kwa jinsi gani Ordinances Ready hufanya kazi?
Kwa kubofya mara kadhaa, Ordinances Ready hutafuta:
- Mti wako wa familia kwa ajili ya ndugu waliofariki wanaohitaji kufanyiwa kazi ya hekaluni.
- Majina yaliyotolewa na waumini wa kata yako na familia ya kigingi.
- Majina yaliyotolewa na waumini wa Kanisa ulimwenguni kote.

Kwa nini nitumie Ordinances Ready?
Ordinances Ready huwasaidia wahudhuriaji hekaluni wenye viwango vyote vya uzoefu kupata majina yaliyo tayari kwa ajili ya hekalu ambayo yamethibitishwa na kuwekewa alama ya vema kwa ajili ya kuondoa rudufu ili kuhakikisha kwamba kazi iko tayari kufanywa. Hata kama unadhani kazi yote ya hekalu imeshafanywa katika familia yako au la, Ordinances Ready itapata mtu kwenye familia yako, ujirani au ulimwenguni ambaye kazi yake inahitaji kukamilishwa.


“Wakati kazi ya hekaluni na historia ya familia ina nguvu ya kuwabariki wale walio upande wa pili wa pazia, inayo nguvu iliyo sawa ya kuwabariki wale walio hai. Inayo nguvu yenye kutakasa juu ya wale ambao wamejiingiza kwenye kazi hiyo.”
Russell M. Nelson
Rais na Nabii wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Nyenzo Zilizopo
Kwa Ajili ya Viongozi wa Kata, Tawi na Kigingi
Gundua nyenzo na mwongozo wa jumla kwa ajili ya uongozi wa kata, tawi na kigingi. Wasaidie waumini wa kanisa wajihusishe katika historia ya familia na ibada za hekaluni.
Jifunze Zaidi ›Kwa Ajili ya Washauri wa Hekalu na Historia ya Familia
Wasaidie waumini kupata uzoefu wa baraka za kuwagundua mababu zao na kufanya ibada za hekaluni kwa niaba yao.
Jifunze Zaidi ›Msaada wa Ziada na Kujifunza
Jifunze zaidi kuhusu Ordinances Ready na tafuta majibu kwa maswali ya ziada.
Jifunze Zaidi ›Ordinances Ready
Ordinances Ready ni njia rahisi zaidi kwa waumini wote kuwakusanya wengine kwa Mwokozi kwa kutafuta kikamilifu majina yanayohusiana na familia ya wale wanaohitaji ibada za kuokoa za hekaluni.
