Wito Wangu: Mshauri wa Kazi ya Hekalu na Historia ya FamiliaFokasi Yangu Ni Ipi?
Kama mshauri wa kata wa hekalu na historia ya familia, unawasaidia watu binafsi na familia kuja kwa Kristo pale wanaposhiriki katika historia ya familia na kazi ya hekalu (Kitabu cha Maelezo ya Jumla 25.2.4).
Hatua hapa chini zitakusaidia kuanza.


"Mafundisho ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kitovu chake ni familia. Muhimu katika mafundisho yetu ya familia ni hekalu. Ibada zinazopokelewa huko hutusaidia kurejea kama familia za milele kwenye uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni."
Rais Dallin H. Oaks, Injili ya Yesu Kristo Inayolenga Familia
Daima Fokasi Kwanza kwa Mwokozi
Unapowaalika watu kuabudu ndani ya nyumba ya Bwana na kufanya ibada kwa ajili ya mababu, anza na Mwokozi. Shiriki jinsi maagano na ibada za hekaluni zinavyotuunganisha kwa Mwokozi, kutusaidia tuhisi mwongozo na faraja na kutuimarisha kwa nguvu na ulinzi Wake.
Kwamba katika kipindi cha maongozi ya Mungu cha utimilifu wa nyakati ataweza kukusanya pamoja vitu vyote katika Kristo, ambavyo vipo mbinguni na ambavyo vipo duniani; hata katika yeye huyo.
Waefeso 1:10
Tumia Ibada zilizo Tayari
Wasaidie waumini watumie Ordinances Ready—njia rahisi zaidi kwa waumini wote kuwakusanya wengine kwa Mwokozi kwa kutafuta kikamilifu majina yanayohusiana na familia ya wale wanaohitaji ibada za kuokoa za hekaluni. Jifunze Zaidi
Ongeza Kile Unachokifahamu
Wahimize waumini wote waongeze tu kile wanachokifahamu kwenye mti wao wa familia—majina, picha, matukio ya maisha, hadithi na kumbukumbu zingine za wapendwa ambao wanaweza kukusanywa kwa Mwokozi.
Viongozi wanaowasaidia waumini wapya na vijana wajiandae kwa ajili ya uzoefu wa ubatizo wao wa kwanza na uthibitisho hekaluni wanaweza kutumiaMsaada wa Jina la Familia.
Nyenzo zinazoweza Kupakulika
SomoKuziunganisha Familia kwa Milele Yote
Muhtasari huu wa somo unaweza kukusaidia kufundisha baraka zinazokuja kutokana na huduma ya hekalu na historia ya familia
Nenda kwenye SomoMafunzo na Nyenzo
Jifunze zaidi kuhusu wito wako na nyenzo zilizopo ili kukusaidia.