Aina za Maeneo ya FamilySearch

Vituo vya FamilySearch
Vituo vya FamilySearch hutoa nyenzo na rasilimali kwa ajili ya kutafiti nasaba yako na historia ya familia. Vinatoa usaidizi binafsi, ufikiaji kwenye kompyuta na tovuti za ziada za historia ya familia, na picha za kumbukumbu za kihistoria ambazo haziwezi kupatikana pengine popote.

Maktaba Washirika
Maktaba washirika wa FamilySearch hutoa rasilimali kama zile zinazopatikana katika kituo cha FamilySearch, kama vile ufikiaji wa mikusanyiko ya kina ya kidijitali ya nasaba ya FamilySearch. Maktaba washirika zinaweza kuwa maktaba ya umma au ya elimu ya juu, makavazi, makumbusho, kituo cha utamaduni, au jumuiya ya nasaba au historia.

Maktaba ya FamilySearch
Ikiwa Jijini Salt Lake, Utah, Maktaba ya FamilySearch ni moja kati ya vitengo vikubwa zaidi vya utafiti wa nasaba ulimwenguni. Kwa kuongezea kwenye wafanyakazi waliopewa mafunzo, inatoa ufikiaji usio na malipo kwenye mkusanyiko mkubwa wa kumbukumbu za nasaba, vitabu, filamu ndogondogo, na rasilimali za kidijitali. Maktaba iko wazi kwa umma bila gharama, na baadhi ya rasilimali zake zinapatikana pia mtandaoni.

Ufikiaji wa FamilySearchMaudhui ya Ziada katika Majengo ya Kanisa
Unaweza kufikia maudhui ya ziada ya kituo cha FamilySearch kwenye kompyuta yako mwenyewe kwenye jengo lolote la mkutano la Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Pakua tu na uhifadhi Maudhui ya Ziada yaliyoongezwa ya Kituo cha FamilySearch kwenyeGoogle ChromeauMozilla Firefox.
