Tunatumaini utafurahia Utafutaji wa Makaburi. Tafadhali kumbuka kwamba kipengele hiki ni cha majaribio na kina usaidizi mdogo.
Utafutaji wa Makaburi
FamilySearch ina kanzidata inayozidi kuongezeka ya makaburi ya kimataifa yaliyounganishwa na nasaba kubwa zaidi ya mtandaoni ulimwenguni. Tafuta kulingana na eneo, jina la makaburi au jina la jamaa ili upate mahali walipozikwa wanafamilia walioaga au mtu mwingine unayevutiwa naye.
Kutembelea makaburi
Makaburi ni mahali pa heshima na ukumbusho, mahali pa kuwaheshimu marehemu na kutambua jinsi maisha yao yalivyogusa maisha yetu. Maeneo ya mazishi, maeneo ya kuchomea maiti na majengo mengine ya ukumbusho hutupatia fursa ya kujifunza zaidi kuhusu mababu zetu na simulizi zao.
Jinsi ya kutumia tovuti hii
Tafuta au uvinjari ili upate makaburi unayopendelea. Kwenye kila ukurasa wa makaburi, utaweza kutafuta mababu zako au watu wengine ambao huenda wamezikwa au wameadhimishwa hapo. Pia utapata taarifa za jumla kuhusu makaburi, kama vile saa na anwani, pamoja na viungo kwenda kwenye ukurasa wa mwanzo wa makaburi kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zinazotolewa.