Kama kiongozi wa Kanisa, unawasaidia watu binafsi na familia kupata amani na nguvu katika Yesu Kristo kadiri wanavyoabudu hekaluni na kuwahudumia mababu zao.

(Kitabu cha Maelezo ya Jumla 25.2)

Daima anza na Mwokozi

Unapowaalika watu kuabudu ndani ya nyumba ya Bwana na kufanya ibada kwa ajili ya mababu, anza na Mwokozi. Shiriki jinsi maagano na ibada za hekaluni zinavyotuunganisha kwa Mwokozi, kutusaidia tuhisi mwongozo na faraja na kutuimarisha kwa nguvu na ulinzi Wake. Jifunze Zaidi

Kwamba katika kipindi cha maongozi ya Mungu cha utimilifu wa nyakati ataweza kukusanya pamoja vitu vyote katika Kristo, ambavyo vipo mbinguni na ambavyo vipo duniani; hata katika yeye huyo.

Waefeso 1:10

Anza na Mwokozi pamoja na Ibada Zilizo Tayari

Wasaidie waumini watumie Ibada Zilizo Tayari—njia rahisi zaidi kwa waumini wote kuwakusanya wengine kwa Mwokozi kwa kutafuta kikamilifu majina yanayohusiana na familia ya wale wanaohitaji ibada za kuokoa za hekaluni. Jifunze Zaidi

Anza na Mwokozi pamoja na Ibada Zilizo Tayari

Anza na Mwokozi kwa kuongeza kile unachokijua

Wahimize waumini wote waongeze tu kile wanachokifahamu kwenye mti wao wa familia—majina, picha, matukio ya maisha, hadithi na kumbukumbu zingine za wapendwa ambao wanaweza kukusanywa kwa Mwokozi.

Viongozi wanaowasaidia waumini wapya na vijana wajiandae kwa ajili ya uzoefu wa ubatizo wao wa kwanza na uthibitisho hekaluni wanaweza kutumiaMsaada wa Jina la Familia.

Jifunze Zaidi

Rasi Russell M. Nelson
“Mahekalu ni sehemu muhimu ya Urejesho wa injili ya Yesu Kristo katika utimilifu wake. Ibada za hekaluni zinajaza maisha yetu kwa nguvu na uwezo usiopatikana kwa njia nyingine yoyote.

Rasi Russell M. Nelson, COVID-19 na Mahekalu

1 kati ya 3