Kuwasaidia Waumini Wapya kwenye Njia ya Agano

"Jukumu letu takatifu ni kuwakubali na kuwakaribisha waumini wapya na wanaorudi. Bwana anapoharakisha kazi Yake, tunapaswa kuwapenda, kuwalea, na kuwahudumia wale wanaoikubali injili Yake."—Mzee Quentin L. Cook, “Bwana Anaharakisha Kazi Yake"

Hatua 4 kwa ajili ya Muumini Mpya Baada ya Ubatizo

Kuchukua hatua hizi nne ndani ya wiki ya kwanza baada ya ubatizo huanzisha njia ya kuziunganisha familia kwa milele yote kupitia ibada na maagano ya hekaluni.

1

Muumini mpya anapaswa kuthibitishwa kuwa muumini wa Kanisa.

2

Muumini mpya anapaswa kupokea kibali cha hekaluni kwa ajili ya ubatizo kwa uwakilishi. Ikiwa ni mwanamume, anapaswa kwanza kutawazwa kwenye Ukuhani wa Haruni.

3

Muumini mpya anapaswa kualikwa kuabudu ndani ya nyumba ya Bwana akiwa na marafiki wa kata, kadiri hali zinavyoruhusu.

4

Viongozi hutumia Msaada wa Jina la Familia ili kuwasaidia waumini kupeleka jina la familia* kwenye nyumba ya Bwana.

*Anza na mwanafamilia anayejulikana, aliyefariki ili kuepusha hitaji la utafiti au teknolojia ya ziada.

Njia za Kuendelea Kuhudumu

Viongozi wanamtambulisha muumini mpya kwa mshauri wa kazi ya hekalu na historia ya familia.

Washauri wa kazi ya hekalu na historia ya familia humsaidia muumini mpya kuongeza kile anachokijua kwenye FamilySearch, jambo ambalo litaongoza kwenye fursa mpya za hekaluni katika Ibada Zilizo Tayari.

Msaidie muumini mpya kuendelea kwenda kwenye nyumba ya Bwana kila mara, pale inapowezekana, ili kumwabudu Mungu na kufanya ibada kwa niaba ya mababu zao.

Msaada wa Jina la Familia kwa Waumini Wapya

Tumia kifaa hiki rahisi ambacho kinaongoza uandaaji na uchapishaji wa kadi za majina ya familia kwa ajili ya ubatizo na uthibitisho hekaluni.

Anza

Kuwahudumia Waumini Wapya Waliobatizwa

Kutana na familia iliyobatizwa karibuni wakienda hekaluni kufanya ubatizo kwa niaba ya wanafamilia wao waliofariki.

Tazama Sasa