Kuwaandaa Watoto na Vijana kwa ajili ya Uzoefu wa Shangwe Hekaluni

"Wakati tulipowatazama vijana wakifanya historia ya familia, tuliwaona wakipata uzoefu wa shangwe ya papo hapo na ongezeko la ujasiri. ... Historia ya familia hutoa ushawishi unaoponya na hakikisho kwamba kila mtu ni wa thamani katika macho ya Baba yetu wa Mbinguni."—President Dallin H. Oaks, 2018 RootsTech Family Discovery Day

Kuimarisha Msingi wenye Kiini kwa Kristo

Jinsi viongozi na wazazi wanavyoweza kuwasaidia watoto wanaofikisha miaka 12 kujiandaa kwa ajili ya ibada na maagano ya hekaluni

Wazazi na viongozi wa Watoto wanaweza kufundisha mara kwa mara kanuni zinazopatikana ndani ya Njoo, Unifuate ambazo zinahusika kwenye maandalizi ya hekaluni (Kiambatisho A; Kiambatisho B).

Wazazi huwasaidia watoto wao kwa kutumia Ibada Zilizo Tayari ili kupokea jina la familia na kuongeza kile wanachokijua kwenyeFamilySearch.org.

Wazazi na viongozi hushiriki kwenye mkutano wa Maandalizi ya Hekaluni na Ukuhani pamoja na watoto.

Msaada wa Jina la Familia kwa ajili ya Vijana

Ona njia ya haraka ya kuwasaidia vijana kupeleka kadi za majina ya familia zao wenyewe hekaluni huku wakiepuka changamoto za jina la mtumiaji na neno siri.

Anza