Burudani ya Historia ya Familia
Jaribu baadhi ya shughuli hizi. Katika muda mfupi utakuwa unafanya ugunduzi wa historia ya familia kwani ni burudani.
Unafanya historia yako ya familia, lakini katika njia mpya tofauti kabisa.
Yote kunihusu Mimi
Je, unadhani maisha yalikuwaje katika mwaka uliozaliwa? Shughuli hii inaelezea uchumi wa wakati huo pamoja na kile kilichokuwa maarufu wakati huo katika muziki, tamthilia na michezo.
Rekodi Hadithi Yangu
Saidia vizazi vijavyo kujifunza kutoka kwenye uzoefu wako wa maisha. Tumia vifaa rahisi kunasa na kuhifadhi rekodi zako kwenye mti wako wa familia au kwenye kompyuta.
Piga Picha Urithi Wangu
Pakia picha na weka uso wako katika mavazi ya kihistoria ya mababu zako. Ongeza mti wako wa familia kufanya mfumo upendekeze mavazi ambayo yanaendana na urithi wako.
Shughuli za Nyumbani
Orodha hii iliyopangiliwa inajumuisha shughuli rahisi ambazo kila mmoja anaweza kufanya, awe au asiwe na kompyuta. Zitamsaidia mtu binafsi au familia kupata uzoefu wa nyakati muhimu za historia ya familia.
Shughuli Zaidi
Je, unatafuta shughuli zaidi za burudani za familia za kujaribu? Ingia kwenye akaunti yako ya FamilySearch kwa ajili ya orodha kamili, ikijumuisha mchezo wa changamoto ya Mababu.