Vipengele Muhimu vya Kumbukumbu za FamilySearch

Vipengele vifuatavyo vitakusaidia kutengeneza mkusanyiko wa urithi wa mafaili mapya na ya zamani ya picha, hadithi, nyaraka na sauti za familia

Tafiti Nguvu ya Tagi za Mada

Mkusanyiko wa kumbukumbu unaweza kuongezeka kwa haraka. Njia nyepesi kukusaidia kupangilia na kufurahia lulu za familia ni kwa kutumia tagi za mada.

Weka tagi ile ile unayopenda kwenye kumbukumbu kadhaa tofauti ili kuzipata kwa urahisi. Zifikirie kama njia fupi kufikia maudhui na mada unazojali.

Je, Umewahi Kushiriki Albamu?

Albamu ni njia nzuri ya kuunganisha na kushiriki Kumbukumbu kuhusu watu au matukio. Watu unaoshiriki nao wanaweza kufurahia kumbukumbu zako moja baada ya nyingine au katika onyesho la picha mwendo.

Kumbukumbu za Kundi kwa mtu, familia, tukio au kipengele kingine chochote. Ni njia nzuri ya kupata hadithi nzima kuhusu babu au maisha ya mwanafamilia. Albamu zinaweza kuwa na aina zote za kumbukumbu—mafaili ya picha, hadithi, nyaraka na sauti—na zinaweza kupangiliwa kwa jinsi utakavyo.

Njia Fupi kufikia Kumbukumbu Zako Pendwa

Alamisho ni viungo kwenye kumbukumbu na albamu ambavyo utapenda kuviangalia tena baadaye. Alamisho zinatunzwa kwenye Galeri.

Rejea kirahisi kwenye kumbukumbu muhimu na hata albamu ambazo ziliongezwa na wengine. Ni njia rahisi ya kutambua picha na hadithi ambazo ni muhimu kwako.

Tengeneza Akaunti ya bure

Ruhusu Watu Wapatikane Kirahisi kwa Tagi Binafsi

Kutagi ni jinsi unavyowatambulisha watu kwenye kumbukumbu. Inachukua dakika moja tu, lakini mara tu inapotagiwa, itakuwa rahisi kwa familia kuipata sasa na baadaye katika Mti wa Familia.

Bofya kwenye picha, au andika jina katika “Nani yuko kwenye kumbukumbu hii” ili kuongeza tagi. Unapomtagi mtu, unaongeza kumbukumbu kwenye wasifu huo.

Tengeneza Akaunti ya bure