Tunawapa mwongozo watu kila mahali ili kuunganika pamoja na familia zao—katika vizazi vyote.

FamilySearch Office, Lehi, Utah, USA
Bure kwa Wote
Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho hutoa FamilySearch bure kwa kila mtu, bila kujali desturi, utamaduni au ushiriki wa dini. Nyenzo za FamilySearch zinawasaidia mamilioni ya watu kote ulimwenguni kugundua urithi wao na kuunganika na wanafamilia.
Kile Tunachokifanya
Tunawasaidia watu kugundua historia ya familia zao kupitia tovuti yetu, app za simu, na msaada kwa watu binafsi katika zaidi ya vituo 5,000 vya historia ya familia.

Ushirikiano wa Ulimwenguni kote
FamilySearch imewekwa wakfu ili kuhifadhi kumbukumbu muhimu za familia na kuzifanya zipatikane bila malipo mtandaoni, kwa kufuata sheria za eneo husika. Kazi yetu ni ya ulimwenguni kote na inahusisha ushirikiano na zaidi ya mashirika 10,000 katika zaidi ya nchi 100. FamilySearch inatafuta kukubaliana na sheria za eneo husika nyakati zote.


















