Ufadhili wa Kanisa
juu ya FamilySearch

Kuunganisha Vizazi
Hisia za muunganiko wa familia zinaweza kutusaidia kushinda panda shuka za maisha. Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho hufadhili FamilySearch ili kuwasaidia watu kupata nguvu kutokana na mahusiano ya familia zao—zilizopita, za sasa na za siku zijazo. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu mafundisho ya Kanisa kuhusiana na familia kwenyeComeUntoChrist.org.

Inamaanisha Nini Kwako
Taarifa binafsi na za familia unazoongeza kwenye FamilySearch hutumika ili kukusaidia wewe kugundua, kuhifahi, na kushiriki hadithi za familia yako. Kamwe haziuzwi kwa kampuni zingine. Taarifa kuhusu familia zilizo hai zinawekwa kwa faragha kwako, huku utondoti wa nasaba wa mababu zako waliofariki zinashirikiwa na watafiti wengine katika jamii ya Mti wa Familia.

Kuboresha Maisha kwa Kila Mtu
Historia ya familia inaweza kuwa chanzo cha maongozi, shangwe, uwazi, rehema, na amani. Tunatumaini kwamba watu wote wa ulimwengu wanaweza kupata uzoefu wa hisia hizi katika maisha yao wanapoendeleza au kutengeneza desturi za familia ambazo zinawasherekea mababu zao.