Makubaliano ya Uwasilishaji wa Maudhui kwenyeFamilySearch

Imesasishwa2023-09-01

FamilySearch International (“FamilySearch”, “nasi”, “sisi”, au sawa na hayo) ni taasisi isiyo ya kibiashara. Uwajibikaji na wajibu wa FamilySearch kuhusiana na uchapishaji na matumizi mengine ya taarifa au nyenzo zitolewazo na FamilySearch.org (“Tovuti” hii) ni kwa ajili ya Vigezo vya Matumiziya Tovuti hii pekee (“Vigezo vya Matumizi”) na kwa Makubaliano haya ya Uwasilishaji wa Maudhui kwenye FamilySearch (“Makubaliano” haya). Makubaliano haya hubainisha na/au huongezea kwenye Vigezo vya Matumizi; hayaondoi Vigezo vya Matumizi. Vyote viwili, Vigezo vya Matumizi na Makubaliano haya vinahusiana kana kwamba vimetajwa kwa uwazi na usahihi, kila moja kwenye lingine. Kwa kuwasilisha, kuchangia au kuweka taarifa yoyote au nyenzo kwenye sehemu yoyote ya Tovuti hii, unakubaliana na Vigezo vya Matumizi na vigezo vyote pamoja na masharti ya Makubaliano haya.

1. Unawajibika kwa Taarifa Uliyowasilisha. Uchaguzi wa kupakia taarifa, maudhui, taarifa za vinasaba, picha, maandishi, nyaraka, sauti/video zilizorekodiwa, majadiliano, maoni, au vitu vingine vyovyote (kwa pamoja au kimoja kimoja), “Maudhui Yaliyowasilishwa”) kwenye tovuti hii ni wajibu wako. Maudhui Yote ambayo unayapakia kwenye Tovuti hii yanaweza kuonekana na kupatikana kwa ajili ya wengine wanapotafuta, kuangalia, kusikia, na kutumia kulingana na Vigezo vya Matumizi na Makubaliano haya. Usiweke chochote ambacho hutataka kiweze kufikiwa na wengine.

2. Haki ya Kuwasilisha.Kwa kuwasilisha Maudhui kwenye Tovuti hii, unathibitisha kwamba unayo haki kisheria ya kuwasilisha Maudhui hayo na kwamba uwasilishaji na matumizi ni kulingana na Vigezo vya Matumizi na Makubaliano haya hayatakiuka haki za faragha ya mtu mwingine, haki za umma, haki za kimikataba, hakimiliki, au haki zingine binafsi. Kwa kuthibitisha haki yako kisheria ya kuwasilisha Maudhui, unakubali uwajibikaji wa kisheria kwa ajili ya matumizi yetu (na wale tuliowaidhinisha) ya Maudhui Uliyoyashiriki.

3. Hakimiliki. Tunazingatia hakimiliki na hakimiliki za kisanaa za wengine. Kumbuka kwamba maudhui, ikijumuisha picha, masimulizi, na uzoefu binafsi, ambayo ni ya muhimu kwako hata kama yamewasilishwa kwenye sehemu ndogo ya Tovuti hii, hubakia kuwa mali ya mtengeneza maudhui au mwasilishaji. Haupaswi kuyazalisha upya bila ruhusa ya mmiliki. Picha za watu walio hai, isipokuwa za watoto wako mwenyewe ambao ni wadogo, hazipaswi kuwasilishwa bila ruhusa yao. Wakati wa kutengeneza sauti/kurekodi sauti, maudhui binafsi yaliyorekodiwa yanapaswa kuwa ya kwako mwenyewe, au kama yametengenezwa na mwingine (kwa mfano, shairi au makala), yanapaswa kutumika kwa ruhusa ya mmiliki.

4. Leseni na HakiTulizopewa. Kwa kuwasilisha Maudhui kwenye Tovuti hii, unaikubalia FamilySearch kwa leseni endelevu isiyozuilika, iliyolipiwa kikamilifu, isiyohitaji mrabaha, ya ulimwenguni kote, isiyotenguliwa, inayoweza kutolewa kwa mwingine ya kutumia Maudhui yoyote na yote ambayo umeyawasilisha au kwa namna nyingine umeyaweka kwenye Tovuti hii, kwa matumizi ya sehemu ya, au sehemu yote, na kwa namna fulani au zote, na kwa muundo wowote au wote wa video/sauti/machapisho ambayo sisi, katika busara yetu, tunaona yanafaa kwa ajili ya uendelezaji wa dhumuni letu la kusaidia historia ya familia na utafiti wa vizazi. Kama sehemu ya leseni hii, unatupatia ruhusa isiyo na ukomo ya kunakili, kuonyesha kwa umma, kurusha, kutumia katika matangazo, kusambaza kwa umma, kutoa leseni kwa mtu mwingine, kutengeneza kazi kutokana na leseni uliyotupatia (ikijumuisha, pasipo ukomo, kwa kuunganisha sehemu ya, au sehemu yote ya Maudhui Uliyoyawasilisha pamoja na yale ya wengine au kwa namna nyingine kurekebisha Maudhui yako), na kwa namna nyingine kuyatumia (na kuwaruhusu wengine kuyatumia) kote ulimwenguni Maudhui yako Uliyoyawasilisha, kwa njia yoyote ambayo tunahisi ni sahihi (kielektroniki au vinginevyo, ikijumuisha kwenye intaneti).

5. Usahihi wa Taarifa Inayowasilishwa. Unakubaliana kutoa kwetu taarifa ya kweli, sahihi, na iliyokamilika. Ikiwa taarifa yoyote unayoitoa kwa utashi wetu itakuwa ya uongo au ya kupotosha, tutakuwa na haki, lakini si kuwajibika, kuchukua hatua yoyote ya kuzuia au kurekebisha ambayo tunahisi itakuwa sahihi kulingana na busara yetu, ikijumuisha kuzuia ufikiaji, ufutaji, na/au uhariri wa sehemu yoyoye ya Maudhui Uliyoyawasilisha.

6. Kujali Watumiaji Wengine. Tunakutaka kuchagua kwa umakini Maudhui Unayoyawasilisha. Tunayo haki ya kuondoa Maudhui yoyote Yaliyowasilishwa ambayo tunaamini, kwa busara yetu wenyewe kwamba, (a) si ya muhimu, (b) ni ya kuleta madhara au kumuaibisha mtu yeyote aliye hai, (c) ni ya kudhihaki, yasiyo na staha, yasiyofaa, yanayotishia au ya kunyanyasa au (d) kwa namna nyingine yanavunja Makubaliano haya, Vigezo vya Matumizi, au Miongozo na Sera Zilizopakiwa. Pia tunaweza kuchukua hatua yoyote, ikijumuisha kuzuia ufikiaji kutokana na kuvunja Makubaliano haya na kuwafahamisha wanaohusika na kuhakikisha sheria zinafuatwa kuhusu shughuli yoyote ambao inaonekana, kwa busara yetu wenyewe, kuvunja sheria zinazotumika.

7. Uchunguzwaji waKiotomatiki. Tunayo haki, bila kuwajibika, kusimamia na kuhariri Maudhui Uliyoyawasilisha. Tunatumia nyenzo za kiotomatiki kuchuja Maudhui Yaliyowasilishwa ya mtu aliye hai ambayo yanaonekana kulingana na busara yetu kukiuka Vigezo vya Matumizi au Makubaliano haya. Ingawa hatufungwi kufanya hili, tunayo haki ya kuhariri Maudhui yako Yaliyowasilishwa kutokana na sababu yoyote au bila sababu.

8. Ulinzi waMawasilisho. Tunakusudia kutumia juhudi zote kulinda uadilifu wa Maudhui yako. Uliyoyawasilisha na kuepuka makosa au kutojumuisha vitu kwenye maudhui ya Tovuti hii. Tunatoa fursa ya kuwasilisha Maudhui kulingana na Vigezo vya Matumizi na Makubaliano haya. Huduma hii na Tovuti hii vinatolewa kama “VILIVYO”, na hatutawajibika au kuwa sehemu ya makosa au kutojumuishwa kwa taarifa kwenye maudhui yoyote ambayo utayapata kwenye Tovuti hii, au kuwajibika kwenye hasara yoyote, au uharibifu wa Maudhui ambayo Uliyawasilisha. Unaweza kuondoa Maudhui yako yoyote Uliyoyawasilisha kutoka kwenye Tovuti hii, lakini hatutatakiwa kuondoa viunganishi au marejeleo ya Maudhui ambayo yameondolewa. Kama nyongeza, unakiri na kukubali kwamba mara tunapokuwa tumetoa kwa wengine Maudhui Uliyoyawasilisha, hatutaweza, na hatutawajibika kuwazuia wao kutoyatumia. Hatuwajibiki juu ya fidia yoyote maalum au ya madhara yoyote kama matokeo ya Uwasilishaji wako wa Maudhui au ukataaji wetu wa kukubali Maudhui Uliyoyawasilisha. Tafadhali ona Vigezo vya Matumizi kwa ajili ya taarifa ya ziada.

9. Sheria za Kulinda Taarifa. Ikiwa uko nje ya Marekani, unakubali kuchakatwa katika nchi ya Marekani taarifa yako yoyote binafsi ambayo umeiwasilisha. Pia unakubali kutii sheria zote zinazohusiana na uhamishaji wa taarifa binafsi kutoka nchi unayoishi kwenda Marekani na kutoka Marekani kwenda nchi unayoishi.

10. Viwango vya Maadili. Tafadhali soma kwa makini sehemu ya Viwango vya Maadili iliyoko kwenye Vigezo vya Matumizi, ambayo, pamoja na sehemu zingine zote za Vigezo vya Matumizi, hutumika kwenye Makubaliano haya.

Imesasishwa 2023-09-01