Masharti na Vigezo kuhusu Ujumbe wa Maandishi
Kama ilivyoboreshwa tarehe 31 Agosti 2021
Maelezo kuhusu Programu/Mpango
FamilySearch.org inatoa huduma ya ujumbe wa maandishi kwako ili kukuwezesha kupokea taarifa kuhusu mababu/wahenga wako, pamoja na habari muhimu na vidokezo vingine. Utaweza kupokea taarifa, vidokezi vya rekodi, au ugunduzi kuhusu mababu/wahenga wako endapo zitapatikana au taarifa mpya au muhimu kama vile rekodi mpya au viashiria vya nasaba/kizazi. Ukijisajili utapokea ujumbe wa uthibitisho kutoka FamilySearch.org. Masafa ya ujumbe wa maandishi yanaweza kutofautiana. Utakapojisajili utathibitisha kuwa umri wako ni zaidi ya miaka kumi na mitatu (13).
Gharama
FamilySearch.org hawatozi ada yoyote kwa kujiunga na kupokea taarifa za maandishi. Inawezekana zikawepo tozo/gharama kwa ujumbe wa maandishi na data/takwimu/habari zinazotozwa na mtoa huduma wako wa kifaa pasiwaya. Gharama za ujumbe na data zinaweza kutumika kwa ujumbe wowote uliotumwa kwako kutoka kwetu au kutoka kwetu Kwenda kwako. Endapo utakuwa na masuali yoyote kuhusu ujumbe wa maandishi au data/takwimu/habari zozote tafadhali wasiliana na mtoa huduma wako wa kifaa pasiwaya.
Kujitoa
Unaweza kujitoa kwenye huduma hii ya ujumbe wa maandishi wakati wowote kwa kujibu STOP. Kufuatia ombi lako hilo, hutapokea tena ujumbe wowote wa maandishi kutoka FamilySearch.org.
Taarifa ya Msaada
Kwa taarifa za ziada, tuma tu ujumbe HELP na utajibiwa na kupatiwa taarifa ya mawasiliano.
Watoa Huduma
Huduma ya MMS haipatikani kwa kila Mtoa Huduma. Wakati mwingine huduma inakosekana au mtandao haupatikani kutokana na barua taka na vipengele vinavyozuia upatikanaji wa huduma ambavyo vimeamilishwa kwenye laini binafsi za simu. Tafadhali wasiliana na mtoa huduma wako wa kifaa pasiwaya mara utakapopata changamoto kama hizo. Fahamu kuwa watoa huduma hawatawajibika endapo ujumbe wa maandishi utachelewa kukufikia au hautakufikia kabisa. Watoa huduma wengine wanaweza kutuma ujumbe wa maandishi kwa kutumia kanuni/alama ya siri/msimbo mfupi au nambari maalumu ya simu yenye ubora wa juu iliyoundwa kwa ajili ya kutuma ujumbe mwingi, wa njia mbili za kuingia na kutoka.
Faragha
Endapo utakuwa na masuali kuhusu faragha, tafadhali tembelea tovuti https://www.familysearch.org/legal/privacy. Data/takwimu/habari zinazopatikana kupitia programu ya msimbo mfupi/alama ys siri hazitatolewa kwa watu wengine wowote kwa madhumuni ya matumizi yao ya kibiashara au kwa sababu nyingine zozote.
Msaada na Taarifa ya Mawasiliano
Ukiwa na masuali kuhusu huduma zinazotolewa, tafadhali tembelea tovuti https://www.familysearch.org/help/helpcenter/.