Pakia Miongozo na Sera

(Ilisasishwa 28-03-2017)

Kanuni kwa ajili ya Picha, Nyaraka na Rekodi za Sauti

Picha, Nyaraka na Rekodi za Sauti za FamilySearch zinapaswa kuwaruhusu watu binafsi kushiriki maudhui ya mababu ambayo huisaidia familia kupata kujuana na kupendana. Kanuni za jumla zifuatazo zinapaswa kutumika:

Yanayofaa. Maudhui yanapaswa kuunga mkono viwango vinavyofaa vya maadili na wema.

Yanayohusika. Maudhui yanapaswa kuunga mkono dhumuni la historia ya familia.

Ya kugeuza mioyo. Maudhui yanapaswa kuwasaidia watu binafsi kupata kuwajua na kuwapenda mababu zao.

Yasiyo ya kibiashara. Maudhui hayapaswi kutangaza au kuuza bidhaa. Hayapaswi kuhujumu haki miliki.

Miongozo ya Sera za Ukaguzi wa Picha, Nyaraka na Rekodi za Sauti

Maudhui HAYAPASWI kuwa na picha, maonyesho, au ufafanuzi wa

1. Utupu au ukosefu wa maadili. Mavazi yanayoonyeshwa katika picha yanapaswa kufungwa zipu na kufungwa vifungo vizuri.

2. Maudhui matakatifu au ya kidini.

a. Mavazi

b. Kaida za dini

c. Baraka ya Kipatriaki

3. Mwanaume au mwanamke kuvaa nguo za jinsia nyingine.

4. Viunganishi vya tovuti za nje (k.m. hakuna URLs).

5. Maneno machafu au ya kukufuru ya aina yoyote.

6. Picha za mwili bila kichwa au uso.

7. Picha za watu wakipeana busu midomoni: watu wakipeana busu kwenye midomo au wakielekea kupeana busu midomoni, bila kujali jinsia, umri, au uhusiano.

8. Kuunga mkono bidhaa au tovuti. Nembo na maneno kwenye mavazi au kwenye mabango, malori, n.k. vitafanyiwa tathmini kila moja kwa upekee.

9. Vitendo, bidhaa, au huduma zisizokuwa halali. Hii inajumuisha madawa.

10. Ufidhuli, ishara au lugha za utovu wa nidhamu.

11. Maonyesho ya chuki au ubaguzi.

12. Vurugu na uharibifu.

a. Picha za vita, uwindaji, na kuvua samaki zitafanyiwa tathmini kila moja kwa upekee.

b. Picha zenye kuonyesha utoboaji wa mwili na tattoo zitafanyiwa tathmini kila moja kwa upekee.

13. Uungaji mkono wa ubaguzi.

14. Uungaji mkono wa uzalishaji wa sasa, kusudi, au shughuli za hisani.

15. Maudhui ya kibiashara. Upekee ni pale tu ambapo:

a. Wewe una umiliki kisheria wa maudhui haya.

b. Haki miliki imeisha muda wake wa matumizi.

Picha, Nyaraka na Rekodi za Sauti hazipaswi kuhaririwa katika njia ya kuzifanya zisiwe sahihi, za uongo, au za kupotosha. Pia, picha yoyote ya kundi ambayo ina mtu hata mmoja ambaye anakiuka yoyote kati ya miongozo iliyoko katika nyaraka hii hairuhusiwi.

Picha, sanaa, au mafaili yaliyopakiwa hivi karibuni au hapo awali au kuundwa kwenye FamilySearch ambayo yanakiuka sera za uwasilishaji yanaweza kuzuiliwa.